Temeke.
Lengo kuu lilikuwa kupata mitazamo kuhusu ndoto na malengo ya vijana pamoja na kuwasilisha maoni hayo kwa DfID ili kulinganisha na maoni yao kuhusu vijana na mahitaji yao.
Baadhi ya washiriki wakiume Tandale wilayani kinondoni wakiwa katika hatua ya kuchora mchoro ambao ulionesha ndoto na malengo yao,ilikuwa hatua ya vijana ya vijana kujua na kutambua ndoto na malengo yao kama vijana.

Kwa Dar es Salaam kulikuwa na jumla ya vijana 60 waliogawanyika katika makundi manne ya vijana 15 kwa kila kundi yakiwa na umri tofauti; kundi la kwanza la wavulana wenye umri kuanzia miaka 15 – 19, kundi la wavulana wenye umri kuanzia miaka 20 – 24, na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa upande wa wasichana. Katika siku mbili za zoezi la ukusanyaji wa maoni ya vijana kuhusu ushiriki wao na fursa zao za kujikimu, tuligawa makundi kwa kufuata umri wao kwa kuanza na wavulana pamoja na wasichana wenye umri kati ya miaka 15 – 19. Siku ya pili tulimazia kwa makundi yaliyobaki ambayo lenye wavulana wa umri kati ya miaka 20 – 24 na wasicha walio katika umri wa miaka 20 – 24.
Baadhi ya washiriki wa kike katika kijiji cha kibada wilayani temeke wakiwa katika mazungumzo ya pamoja kueleza ndoto na malengo yao kama vijana.
No comments:
Post a Comment