Saturday, 18 April 2015

SHINDANO LA UANDISHI WA INSHA

Ungependa kushiriki kwenye uandishi wa insha na kuibuka MSHINDI? Kama jibu ndio, FURSA ndio hii.
TAMASHA VIJANA kupitia FETAPRO (Focus on Education Tanzania Program) wanakuletea mashindano ya uandishi wa insha kwa wanafunzi wa shule za Sekondari zifuatazo;-
Yusuf Makamba, Mabibo, Kigogo, Mburahati, Makurumla, Turiani, Hananasif, Kambangwa, Makumbusho, Salma Kikwete na Manzese. Zawadi kidogo zitatolewa kwa wanafunzi watano watakaofanya vizuri, ikiwa kama sehemu ya kuchochea hisia za usomaji wa kiuchambuzi.
Mashindano yatafunguliwa rasmi tarehe 20 Aprili 2015 na kufungwa tarehe 8 May 2015. Kama wewe si mwanafunzi wa shule tajwa hapo na ungependa kushiriki tafadhari wasiliana kupitia 0756 366 650 au hpukey@rocketmail.com kujua namna gani unaweza kushiriki katika mashindano haya ya uandishi wa insha.





No comments:

Post a Comment